Hosea 7


1 akila mara nilipotaka kumponya Israeli,
dhambi za Efraimu zinafichuliwa
na maovu ya Samaria yanafunuliwa.
Wanafanya udanganyifu,
wevi huvunja nyumba,
maharamia hunyang’anya barabarani,

2 blakini hawafahamu kwamba
ninakumbuka matendo yao yote mabaya.
Dhambi zao zimewameza,
ziko mbele zangu siku zote.


3 c“Wanamfurahisha sana mfalme kwa maovu yao,
wakuu wao kwa uongo wao.

4 dWote ni wazinzi,
wanawaka kama tanuru
ambayo moto wake mwokaji hana haja ya kuuchochea
kuanzia kukanda unga
hadi umekwisha kuumuka.

5 eKatika sikukuu ya mfalme wetu
wakuu wanawaka kwa mvinyo,
naye anawaunga mkono wenye mizaha.

6 fMioyo yao ni kama tanuru,
wanamwendea kwa hila.
Hasira yao inafoka moshi usiku kucha,
wakati wa asubuhi inalipuka
kama miali ya moto.

7 gWote ni moto kama tanuru;
wanawaangamiza watawala wao.
Wafalme wake wote wanaanguka,
wala hakuna yeyote kati yao aniitaye mimi.


8 h“Efraimu anajichanganya na mataifa;
Efraimu ni mkate ambao haukuiva.

9 iWageni wananyonya nguvu zake,
lakini hafahamu hilo.
Nywele zake zina mvi hapa na pale,
lakini hana habari.

10 jKiburi cha Israeli kinashuhudia dhidi yake,
lakini pamoja na haya yote
harudi kwa Bwana Mwenyezi Mungu wake
wala kumtafuta.


11 k“Efraimu ni kama hua,
hudanganywa kwa urahisi na hana akili:
mara anaita Misri,
mara anageukia Ashuru.

12 lWakati watakapokwenda,
nitatupa wavu wangu juu yao;
nitawavuta chini waanguke
kama ndege wa angani.
Nitakaposikia wakikusanyika pamoja,
nitawanasa.

13 mOle wao, kwa sababu
wamepotoka kutoka kwangu!
Maangamizi ni yao
kwa sababu wameniasi!
Ninatamani kuwakomboa,
lakini wanasema uongo dhidi yangu.

14 nHawanililii mimi kutoka mioyoni mwao,
bali wanaomboleza vitandani mwao.
Hukusanyika pamoja kwa ajili ya nafaka na divai mpya,
lakini hugeukia mbali nami.

15 oNiliwafundisha na kuwatia nguvu,
lakini wanapanga mabaya dhidi yangu.

16 pHawamgeukii Yeye Aliye Juu Sana,
wako kama upinde wenye kasoro.
Viongozi wao wataanguka kwa upanga
kwa sababu ya maneno yao ya jeuri.
Kwa ajili ya hili watadhihakiwa
katika nchi ya Misri.
Copyright information for SwhKC